Jinsi ya kujisajili kama .tz Reseller

Reseller ni programu inayokuwezesha kusajili domains za .tz bila kuwa registrar wa TCRA. Programu hii inakuwezesha kusajili domains moja kwa moja kutoka kwenye System yako na kukupunguzia mlolongo ya kazi.

Kwa kutumia programu ya WHMCS, wateja wataweza kujisajili moja kwamoja kwenye website yako, na kipachiko chetu (addon module) itafanikisha mawasiliano kati ya System mbili na kuwezesha kusajili domain.

Jinsi ya kujiunga:

  1. Kama bado hauna akaunti, Jiunge na Duhosting  https://www.duhosting.co.tz/billing/register.php 
  2. Hakikisha unamiliki domain kumi zilizo hai (Active domains) au weka salio lenye thamani ya domain kumi Tsh 210,000/=
  3. Tuma Ticket kwenye idara ya Domains & .tz Resellers au whatsapp kuomba kujiunga na reseller program, utapewa API key utakayoitumia kuactivate module ya reseller wakati unafanya settings
  4. Doanload module ya reseller https://duhosting.co.tz/Duhosting.zip
  5. Iweke module kwenye folder la whmcsfolder/modules/registrars
  6. Nenda kwenye Setup->products/Services->Domain Registrars

 

7. Chagua Duhosting registrar, bonyeza activate

 

8. Weka username: email unayotumia kwenye client area na API Key uliyopatiwa na Duhosting Support team

 

9. Baada ya kumaliza hatua hii, hakikisha unafanya setup ya bei za domain, pia ukichagua Duhosting kama Registrar kwenye sehemu ya Registrar

 

Hadi hapo, umeshakamilisha kufanya setup ya Domain yako, kama utakuwa na shida yoyote, usisite kuwasiliana nasi.

  • reseller, .tz, domain, tanzania, reselldomain
  • 1 Users Found This Useful
Was this answer helpful?